123
" Wakati Ford Bronco inatoka katika Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals S.A de C.V. (kilichomilikiwa na mkurugenzi mkuu wa 'methamphetamine' wa Kolonia Santita mfanyabiashara wa Kichina kutoka Chaling, katika jimbo la Hunan, kusini ya kati ya China, Li Dongyang; na mkurugenzi wa usalama wa Kolonia Santita kutoka Lomas de Chapultepec, Mexico City, Gortari Manuel) Daniel Yehuda na Radia Hosni, waliokuwa wakipiga picha kila kitu kilichokuwa kikiingia na kutoka kiwandani kwa ajili ya ripoti ya upelelezi wao ya baadaye, waliiona. Lakini, hawakujua kama ilikuwa ikienda Varsovia kumuua Murphy na Sajini Mogens.
Bronco ilipofika Varsovia ilisimama kwa fujo mbele ya SUV ya msafara wa Mtoto wa Rais Debbie Patrocinio Abrego, aliyekuwa ndani ya Mgahawa wa Angus akicheza muziki wa 'mariachi' na John Murphy, huku Mogens akilinda usalama wa kamanda wake na usalama wa baa nzima. Kabla majambazi wa Kolonia Santita hawajaleta madhara au fujo yoyote kwa Vijana wa Tume, polisi walifika eneo lile haraka ilivyowezekana! Kwa msaada wa walinzi wa Debbie! Wale majambazi walipekuliwa na kukutwa na bastola moja ya Akdal Ghost, bunduki mbili za AK-47, na picha nne za Vijana wa Tume ndani ya gari yao. Polisi waliwakamata na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Tume ya Dunia kilichopo Zona Rosa, Mexico City. "
― Enock Maregesi
124
" Kofia za chuma au sandarusi zenye uwezo wa kukwepesha risasi za wadunguzi na kuzuia mpaka risasi tatu za AK-47, ijapokuwa zimetengenezwa kuzuia risasi moja tu, ni miongoni mwa vitu 17 vilivyobebwa na makomandoo wa Tume ya Dunia; wakati wakitekeleza Operesheni ya Kifo au Ushindi Kamili (operesheni ndogo ya Operation Devil Cross ya Tume ya Dunia) katika Msitu wa Benson Bennett, Salina Cruz, Oaxaca, nchini Meksiko. Thamani ya vitu vya komandoo mmoja wa EAC ('Executive Action Corps') akiwa vitani ni zaidi ya dola za Kimarekani 65,000; ikiwa ni pamoja na magwanda ya jeshi ('Ghillie Suits'), kofia za chuma, miwani ya kuonea usiku (yenye uwezo wa kubinuka chini na juu), redio na mitambo ya mawasiliano migongoni mwao juu ya vizibao vya kuzuia risasi, vitibegi vya msalaba mwekundu ('Blowout kits' – katika mapaja ya miguu yao ya kulia, ndani yake kukiwa na pisto na madawa ya huduma ya kwanza), vitibegi vya kujiokolea ('Evasion Kits' – katika mapaja ya miguu yao ya kushoto, ndani yake kukiwa na visu na pesa na ramani ya Meksiko) na bunduki za masafa marefu. "
― Enock Maregesi
125
" Vitibegi vya makomandoo wa Tume ya Dunia (vitibegi vya msalaba mwekundu na vitibegi vya kujiokolea) vilikuwa na vifaa maridadi vya kisasa kama vile pisto, visu, madawa ya huduma ya kwanza, kalamu za Inka, ramani za Meksiko, tochi ndogo zenye mwanga mkali za Cyba-Lite, Vioo vya TOPS, vibiriti vya Firesteel, pasi za kusafiria, pesa na vipenga vyenye viwango vya sauti vya desabo 126. Kipenga chenye kiwango cha sauti cha desabo 126 kinaweza kupasua ngoma za masikio ya adui, na kuwajulisha Vijana wa Tume mwenzao alipo hivyo kwenda haraka na kumpa msaada. "
― Enock Maregesi
135
" Usiwe na wasiwasi, Peter. Hizo ni hisia zangu tu. Huwezi kuwa mpelelezi. Lakini, kusema ule ukweli, ningependa sana kuonana na John Murphy. Kuna kazi binafsi ningependa kumpa. Wewe unatoka Afrika, hujawahi kumwona?” Debbie alizidi kumshtua Murphy.
“Nani?” Murphy aliuliza huku akitabasamu.
“John Murphy wa Afrika.”
“Sijawahi kumwona. Mbona unamuulizia hivyo?”
Debbie alitulia. Kisha akarusha nywele ili aone vizuri.
“Nampenda sana!”
“Kwa nini?”
“Simpendi kwa mahaba, lakini.”
“Ndiyo. Kwa nini?”
“OK. Nampenda kwa kipaji chake. Alichopewa na Mungu, cha ujasusi. Kusaidia watu.”
“Ahaa!” Murphy alidakia, sasa akifikiri sana.
“Murphy ana mashabiki wengi hapa Meksiko bila yeye mwenyewe kujua, kwa sababu ya kupambana na wahalifu wa madawa ya kulevya – hasa wa huku Latino. Tatizo lake haonekani. Wengi hudhani ni hadithi tu, kwamba hakuna mtu kama huyo hapa duniani.”
“Hapana! Murphy yupo! Ni mfanyabiashara maarufu huko Tanzania. Lakini ndiyo hivyo kama unavyosema ... Haonekani! "
― Enock Maregesi , Kolonia Santita
136
" Lakini kabla Rais hajaendelea kuongea, na ‘John Murphy wa Kolonia Santita’, Mogens aliruka na kumnyang’anya simu.
“Ambilikile,” Mogens aliita, akiangalia saa.
“Brodersen,” Sauti ya upande wa pili ilijibu, baada ya sekunde kumi.
“60111906,” Mogens alisema, baada ya sekunde kumi.
“57121906,” Sauti ya upande wa pili ikajibu, baada ya sekunde kumi.
“Jumapili,” Mogens aliendelea, baada ya sekunde kumi.
“Ijumaa,” Sauti ya upande wa pili ikajibu, baada ya sekunde kumi.
John Murphy wa Kolonia Santita aliposema ‘Ijumaa’, Mogens aliunda kicheko na kurusha mkono katika matundu ya kuongelea ya simu ... "
― Enock Maregesi , Kolonia Santita