Home > Author > Enock Maregesi >

" Jicho ni kiungo cha ajabu zaidi kuliko viungo vyote katika mwili wa mwanadamu baada ya ubongo. Jicho moja linatengenezwa na viungo vidogovidogo zaidi ya milioni mbili, vinavyofanya kazi kwa pamoja bila kukosea. Macho yana nguvu ya ajabu. Huu ni wito kwa akina mama wanaonyonyesha: Usizungumze maneno mabaya mtoto wako mchanga anapokuangalia machoni wakati ananyonya ziwa lako. Neno lolote utakalomwambia, zuri au baya, pamoja na kwamba amekuwa akisikia sauti yako kwa miezi kadhaa akiwa tumboni, litajirekodi katika akili yake isiyotambua bila wewe au yeye mwenyewe kujua. Neno hilo litakuja kumuathiri baadaye atakapokuwa mkubwa. Atakapopevuka, atakapokuwa na uwezo wa kupambanua mambo, atakuwa anaota na kuwaza kile ambacho ulikuwa ukimwambia alipokuwa tumboni; na alipokuwa akinyonya na kukukodolea macho. "

Enock Maregesi


Image for Quotes

Enock Maregesi quote : Jicho ni kiungo cha ajabu zaidi kuliko viungo vyote katika mwili wa mwanadamu baada ya ubongo. Jicho moja linatengenezwa na viungo vidogovidogo zaidi ya milioni mbili, vinavyofanya kazi kwa pamoja bila kukosea. Macho yana nguvu ya ajabu. Huu ni wito kwa akina mama wanaonyonyesha: Usizungumze maneno mabaya mtoto wako mchanga anapokuangalia machoni wakati ananyonya ziwa lako. Neno lolote utakalomwambia, zuri au baya, pamoja na kwamba amekuwa akisikia sauti yako kwa miezi kadhaa akiwa tumboni, litajirekodi katika akili yake isiyotambua bila wewe au yeye mwenyewe kujua. Neno hilo litakuja kumuathiri baadaye atakapokuwa mkubwa. Atakapopevuka, atakapokuwa na uwezo wa kupambanua mambo, atakuwa anaota na kuwaza kile ambacho ulikuwa ukimwambia alipokuwa tumboni; na alipokuwa akinyonya na kukukodolea macho.