Home > Author > Enock Maregesi
161 " Askari wa Kirumi alimchoma Yesu mkuki ili andiko litimie. Askari huyo ambaye Biblia haikumtaja jina kwa sababu zilizoko nje ya uwezo wetu, alivyoona kweli amepona na ameona alishuhudia, na ushuhuda wake ulitoka moyoni, ili nasi tupate kusadiki. Wauaji wa Kirumi walipoona kwamba wale wezi waliosulubiwa pamoja na Yesu walikuwa bado hawajakata roho, waliwavunja miguu ili washindwe kupumua na hivyo kuharakisha kifo chao. Kwa upande wa Yesu, waliona alishapoteza fahamu na labda alishafariki. Kuthibitisha hilo askari wa Kirumi alirusha mkuki, nao ukatoboa utando unaozunguka moyo wa Yesu na mapafu ya Yesu, na damu na maji kutoka. Lakini yote hayo yalishatabiriwa miaka mingi kabla ya Yesu: ‘Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa’ na ‘Nao watamtazama yeye ambaye walimchoma’. "
― Enock Maregesi
162 " Soma vitabu visivyopendeza vilivyoandikwa na waandishi mahiri. "
163 " Meja Jenerali U Nanda, 60, Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, alizaliwa Jumamosi ya tarehe 19/03/1932 kandokando ya mto huko Maubin nchini Bama. Yeye na familia yake ni waumini wa dini ya Ubuda. Mke wake, Daw Aung Phyu, ana miaka 57. Alizaliwa Jumapili ya tarehe 20/10/1935. Nanda na Aung Phyu wana watoto watatu. Ko Mahn Thiri (wa kiume na wa kwanza kuzaliwa) ana miaka 37. Alizaliwa Alhamisi ya tarehe 08/12/1955. Yeye na familia yake wanakaa nchini Tailandi. Ma Nang Nyi ni mtoto wa pili wa familia ya Nanda na Aung Phyu. Alikufa kwa madawa ya kulevya Jumamosi ya tarehe 12/05/1980 akiwa na miaka 23. Alizaliwa Jumamosi ya tarehe 06/04/1957. Miaka miwili baadaye mpenzi wake wa kiume, Ko San Pe, alikufa kwa madawa ya kulevya pia Jumatano ya tarehe 21/07/1982 akiwa na miaka 25. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 29/01/1957. Ma Thida Wai Aung ni wa mwisho kuzaliwa. Ana miaka 34. Alizaliwa Jumatano ya tarehe 23/07/1958. Anakaa Rangoon na mume wake wa miaka sita na watoto wawili, wa kike na wa kiume. Saw Saya (Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, kutoka katika kabila la Karen) ndiye aliyempa taarifa U Nanda za kikao cha dharura cha Tume ya Dunia. Ana miaka 54. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 01/03/1938. "
164 " Usiangalie nyuma kujutia vitu ulivyovifanya, angalia nyuma kujifunza kutokana na makosa uliyofanya. "
165 " Msamaha si kwa ajili ya watu wenye mabawa ya kuku, ni kwa ajili ya watu wenye macho ya tai. Kua kuujua msamaha. "
166 " Debbie alilia. Alilia kwa nguvu zake zote. Alijua tayari alishampoteza Murphy na yote yale huenda alisababisha yeye. Bila kujuana na Vijana wa Tume huenda wasingepigwa. Debbie Hakukata tamaa. Alikumbuka kitu halafu akamwita dereva. Alimwomba dereva amkimbize Roma Notre haraka ilivyowezekana. Alidhani alijua majambazi walikokuwa wakikimbilia na kuna kitu alitaka kufanya. Dereva akamkubalia na kuondoka kuelekea Roma Notre. Njiani Debbie hakuacha kulia. Aliwaza alivyompoteza Marciano, akawaza kumpoteza na Murphy. Jibu alilolipata ni kumwokoa Murphy kwa gharama yoyote ile. "
― Enock Maregesi , Kolonia Santita
167 " Sina nyemi na mwanamke mwenye sura nzuri na tabia mbaya. Nina nyemi na mwanamke mwenye sura mbaya na tabia nzuri, au mwanamke mwenye sura nzuri na tabia nzuri. Mwanamke wa kuoa sitampenda nitampendelea. "
168 " Uwezekano wa watoto wa ukoo mmoja kuoana ni mkubwa kwa sababu damu ina nguvu ya uvutano. Kuhakikisha kwamba familia zinafahamiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ni jukumu la wazazi. "
169 " Dunia – Mfumo wa Jua wa Sol – Solar Interstellar Neighborhood – Njiamaziwa – Local Galactic Group – Virgo Supecluster – Local Supercluster – Ulimwengu unaoonekana – Ulimwengu. Huu ndiyo ukoo wa dunia yetu. Chochote alichokifanya Yoshua kilitokea katika ukoo huu. "
170 " Shetani hawezi kusoma ndani ya mioyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Ukionyesha tamaa ya chuki, Shetani atakupa chuki. Ukionyesha tamaa ya upendo, Mungu atakupa upendo. Kama kuna ubishi kati ya moyo wako na akili yako, fuata moyo wako. "
171 " Manabii wa uongo wana dhambi kuu tatu: tamaa ya ngono, uasi dhidi ya mamlaka ya Kristo, na dharau kwa Shetani. "
172 " Tunazaliwa na kufa. Lakini hatujui tunakotoka. Wala hatujui tunakokwenda. Huenda tunatoka na kwenda katika dunia nyingine, ya ulimwengu mwingine, hivyo kutufanya wageni wa dunia yetu wenyewe. Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta. "
173 " Chumvi si dawa ya kuzuia wachawi au dawa ya kuzuia nguvu kutoka ulimwenguni. Chumvi inazuia wachawi, lakini vilevile inazuia bahati. Dawa halisi ya kuzuia wachawi ni Mwenyezi Mungu. "
174 " Kamwe usikubali kuwa mvivu, wala usikubali kuwa mlaodikia. Usikubali starehe za dunia hii kuwa kikwazo cha maendeleo yako ya kiroho ya kadari ya maisha yako. Palilia bustani yako ya kiroho, kuondoa magugu ambayo ni raha za dunia hii. "
175 " Kama kuna jambo la muhimu unapaswa kufanya kwa ajili ya kadari ya maisha yako na kipindi hichohicho kuna kipindi kizuri cha televisheni unakisubiria, au simu ya umbea, au kinanda cha shida, palilia bustani yako ya kiroho kwa kuachana na televisheni na simu na kufanya jambo la msingi kwa ajili ya maisha yako. "
176 " Damu ya Mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi. Mungu hauwi, Anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Ukifunikwa na damu ya Mwanakondoo Shetani, ambaye ni wakala, hatakuona. Lakini Mungu atakuona. Bila kafara ya damu hakuna msamaha wa dhambi. Bila kafara ya damu hakuna mafanikio. "
177 " Shetani anapenda damu kumtumia Mungu kwa faida yake kama vile Mungu anavyomtumia Shetani kwa faida yake. Mungu anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu, na Shetani anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Mungu anaishi ndani ya damu na damu ina nguvu kuliko Shetani. "
178 " Mungu ni mtakatifu na kwa maana hiyo hatendi dhambi. Hivyo, hauwi wala hatesi. Tunajiua na kujitesa wenyewe. Ametupa hiari ya kuchagua mema au mabaya. Lakini anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu pale tunapoenenda sawasawa na machukizo yake. Damu ina nguvu kuliko Shetani na ina nguvu kuliko kuzimu. Unapojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani hataweza kukuona. Hivyo, hataweza kukudhuru. Lakini usipojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani atakuona. Hivyo, atakudhuru. Atakudhuru kwa sababu Mungu atakuwa ameruhusu akudhuru, kwa sababu ya uhuru wa kuchagua mema au mabaya aliotupatia, ijapokuwa ana uwezo wa kuzuia asikudhuru. Kwa mtindo huo Mungu anakuwa ametoa adhabu kwa binadamu. "
179 " Shetani naye anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu kwa sababu Shetani siku hizi anaishi makanisani na misikitini. Anamtumia Mungu kwa maana ya kutuingiza dhambini huku tunaona, tukiwa mbele ya uwepo wa Mungu tunayemwabudu. "
180 " Lolote unalolifikiria yupo mtu mahali fulani duniani ameshalifikiria. "