Home > Author > Enock Maregesi >

" Vijana wa Tume walipofika kambini chini ya ulinzi mkali wakiwa na Kahima, polisi wengi walionekana kuwapigia saluti lakini wakubwa wao wakawakataza na kuwambia wao walikuwa watu wa kawaida kama wao. Walisindikizwa na lundo la polisi mpaka ndani ya jumba la utawala Murphy alimokuwa ameuhifadhi mwili wa Radia. Walipofika walishtuka, na hata kuwashangaza polisi. Mwili wa Radia haukuwepo! Walitafuta kila sehemu, na kuwambia polisi wawasaidie kutafuta, lakini Radia alishapotea. Murphy alipata wazo na kutoka nje, kwa kukimbia, polisi wengi wakimfuata; mpaka katika helikopta ya DEA ambapo alifungua mlango na kuingia ndani. Ndani ya helikopta hakukuwa na mtu! "

Enock Maregesi , Kolonia Santita


Image for Quotes

Enock Maregesi quote : Vijana wa Tume walipofika kambini chini ya ulinzi mkali wakiwa na Kahima, polisi wengi walionekana kuwapigia saluti lakini wakubwa wao wakawakataza na kuwambia wao walikuwa watu wa kawaida kama wao. Walisindikizwa na lundo la polisi mpaka ndani ya jumba la utawala Murphy alimokuwa ameuhifadhi mwili wa Radia. Walipofika walishtuka, na hata kuwashangaza polisi. Mwili wa Radia haukuwepo! Walitafuta kila sehemu, na kuwambia polisi wawasaidie kutafuta, lakini Radia alishapotea. Murphy alipata wazo na kutoka nje, kwa kukimbia, polisi wengi wakimfuata; mpaka katika helikopta ya DEA ambapo alifungua mlango na kuingia ndani. Ndani ya helikopta hakukuwa na mtu!