Home > Topic > Kuamini
1 " Imani ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana na hupeleka watu kwenye ukweli. Kuamini hupotosha, na ni nia ya kudharau kinachoweza kujulikana. "
― Enock Maregesi
2 " Kuamini (mbali na imani, ambayo ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana) ni kwa ajili ya vitu usivyoweza kuvielezea. Unaamini kwamba siku moja dawa ya UKIMWI au saratani itapatikana mahali fulani, ilhali huwezi kufanya majaribio ya kisayansi kulithibitisha hilo. Unaweza kusubiri hata miaka mia, lakini kama bado dawa haijapatikana, unaweza kusubiri hata miaka mingine mia. Kuamini ni kujifanya kujua (na mara nyingi kujifanya kujua ni uongo) na kuamini hakuhitaji maarifa. Kujua kunahitaji maarifa na ni kuamini unakoweza kukuthibitisha. Ukiniuliza kama simu yangu ipo mfukoni nitakwambia ndiyo ipo, kwa sababu nitaingiza mkono mfukoni na kuitoa na kuiona. Siamini kama ipo mfukoni, najua. "
3 " Kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa raha ni rahisi kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa shida, na utahitaji imani kuendelea kumwamini wakati wa dhiki. Vipindi vigumu katika maisha yetu hutokea kwa kila mmoja wetu. Kuamini ya kwamba Mungu ana makusudi ya lazima kukuondolea vikwazo katika maisha yako ni vigumu sana wakati mwingine, lakini imani ndicho kitu cha muhimu zaidi unachotakiwa kuwa nacho katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Amani ya Mungu, ambayo huzidi hekima na maarifa yote ya kibinadamu, ni kuliamini neno la Mungu kwamba ni la kweli. Bila imani hutaweza kumfurahisha Mungu. Imani ni ufunguo wa nguvu, uwezo na neema ambavyo Mungu ametupangia. Kwa ufupi, Mungu ni mkubwa kuliko wewe na matatizo yako. "