Home > Author > Enock Maregesi >

" Mungu si wa kudhihakiwa (Wagalatia 6:7)! Katika maneno kadhaa ya Biblia, anasema bila masihara kabisa kwamba yeye ni Mungu mwenye wivu (Kutoka 34:14; Kumbukumbu la Torati 6:4-15) – Yeye si wa kuabudiwa kama mungu mwingine yeyote yule (Kumbukumbu la Torati 12:3-4, 30-31). Alipowaagiza watu wake wateule Israeli kwa njia ya ibada yake, aliwaonya wasiongeze juu ya kile alichokuwa amewapa wala wasipunguze chochote (Kumbukumbu la Torati 4:2; 12:32; angalia pia Ufunuo 22:18-19).

Kwa mfano, angalia hasira yake kuu wakati wana wa Israeli walipojaribu kumwabudu kupitia Ndama wa Dhahabu (Kutoka 32:1-9). Walitangaza kuwa ilikuwa sikukuu ya Bwana (mstali wa 5), lakini Mungu hakulithamini hilo! Alikuwa na hasira kali juu ya ibada ya sanamu za watu, kiasi kwamba alifikiria kuangamiza taifa zima na kuanza upya na familia ya Musa.

Mungu huyohuyo – Yahweh, Bwana wa Agano la Kale – akawa Yesu Kristo! Je, Mwokozi wetu atakubali kuabudiwa kwa namna yoyote ambayo misingi yake imejikita kwenye uongo? Hapana! Na hili kwa vyovyote vile limezingatia mila na desturi zisizo za kibiblia (labda tunaweza kusema za “kipagani”) ambazo zimechukua nafasi ya maadhimisho ya kafara na ushindi wa kishindo wa Yesu Kristo. "

Enock Maregesi


Image for Quotes

Enock Maregesi quote : Mungu si wa kudhihakiwa (Wagalatia 6:7)! Katika maneno kadhaa ya Biblia, anasema bila masihara kabisa kwamba yeye ni Mungu mwenye wivu (Kutoka 34:14; Kumbukumbu la Torati 6:4-15) – Yeye si wa kuabudiwa kama mungu mwingine yeyote yule (Kumbukumbu la Torati 12:3-4, 30-31). Alipowaagiza watu wake wateule Israeli kwa njia ya ibada yake, aliwaonya wasiongeze juu ya kile alichokuwa amewapa wala wasipunguze chochote (Kumbukumbu la Torati 4:2; 12:32; angalia pia Ufunuo 22:18-19). <br /><br />Kwa mfano, angalia hasira yake kuu wakati wana wa Israeli walipojaribu kumwabudu kupitia Ndama wa Dhahabu (Kutoka 32:1-9). Walitangaza kuwa ilikuwa sikukuu ya Bwana (mstali wa 5), lakini Mungu hakulithamini hilo! Alikuwa na hasira kali juu ya ibada ya sanamu za watu, kiasi kwamba alifikiria kuangamiza taifa zima na kuanza upya na familia ya Musa. <br /><br />Mungu huyohuyo – Yahweh, Bwana wa Agano la Kale – akawa Yesu Kristo! Je, Mwokozi wetu atakubali kuabudiwa kwa namna yoyote ambayo misingi yake imejikita kwenye uongo? Hapana! Na hili kwa vyovyote vile limezingatia mila na desturi zisizo za kibiblia (labda tunaweza kusema za “kipagani”) ambazo zimechukua nafasi ya maadhimisho ya kafara na ushindi wa kishindo wa Yesu Kristo.