Home > Author > Enock Maregesi >

" John Murphy alifika Moscow tarehe 1/11/1992 saa 11 alfajiri akitokea Cairo, Misri. Wakati huo Moscow kulikuwa na baridi sana. Teksi yake ilipofika Teatralny Proezd, upande wa kusini wa Hoteli ya Metropol – karibu na mojawapo ya minara ya mwanzo ya Kitay-gorod, kitovu kikuu cha biashara cha Moscow ya kale – kwa matatizo ya injini; magaidi wanne, waliokuwa wakimfuatilia kwa gari aina ya Bentley Continental S nyeusi – iliyokuwa na namba za kitemi za B 001 BB 77 RUS mali ya Kiongozi wa CS-Moscow Dmitri Olegushka – toka Uwanja wa Ndege wa Sheremetyevo II wa kaskazini-magharibi mwa jiji la Moscow, waliendelea mbele na kusimama mkabala na Jumba la Maonyesho ya Tamthilia la Bolshoy; kisha wawili kati yao wakashuka na kuingia ndani ya kioski, wawili wakibaki ndani ya gari kuhakikisha John Murphy hawapotei. Magaidi hao wa CS-Moscow, Tawi la Kolonia Santita la Urusi na nchi zote za Ulaya ya Mashariki na baadhi ya nchi za Ulaya ya Kusini, walijua Murphy alishawahisi. "

Enock Maregesi


Image for Quotes

Enock Maregesi quote : John Murphy alifika Moscow tarehe 1/11/1992 saa 11 alfajiri akitokea Cairo, Misri. Wakati huo Moscow kulikuwa na baridi sana. Teksi yake ilipofika Teatralny Proezd, upande wa kusini wa Hoteli ya Metropol – karibu na mojawapo ya minara ya mwanzo ya Kitay-gorod, kitovu kikuu cha biashara cha Moscow ya kale – kwa matatizo ya injini; magaidi wanne, waliokuwa wakimfuatilia kwa gari aina ya Bentley Continental S nyeusi – iliyokuwa na namba za kitemi za B 001 BB 77 RUS mali ya Kiongozi wa CS-Moscow Dmitri Olegushka – toka Uwanja wa Ndege wa Sheremetyevo II wa kaskazini-magharibi mwa jiji la Moscow, waliendelea mbele na kusimama mkabala na Jumba la Maonyesho ya Tamthilia la Bolshoy; kisha wawili kati yao wakashuka na kuingia ndani ya kioski, wawili wakibaki ndani ya gari kuhakikisha John Murphy hawapotei. Magaidi hao wa CS-Moscow, Tawi la Kolonia Santita la Urusi na nchi zote za Ulaya ya Mashariki na baadhi ya nchi za Ulaya ya Kusini, walijua Murphy alishawahisi.