Home > Topic > sababu
1 " Wanasayansi wanasema hakuna Mungu kwa sababu hawawezi kumwona wala kumgusa. Lakini nao hawana akili kwa sababu hawawezi kuiona wala kuigusa. "
― Enock Maregesi
2 " Mungu ana uwezo wa kukuwekea ulinzi kulia na kushoto yaani anayekulinda naye ana mlinzi wake. Lakini wakati mwingine anaacha ufuate kile ambacho moyo wako unataka kwa sababu hataki kukulazimisha ijapokuwa uwezo huo anao. Mungu hakukuumba kuwa roboti. Alikuumba kuwa huru kuchagua mema au mabaya usije ukamlaumu baadaye kwamba ulimchagua yeye kwa sababu hukuwa na uhuru. Msikilize Roho wa Mungu, kabla na katika kila jambo unalofanya. "
3 " Kuamini (mbali na imani, ambayo ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana) ni kwa ajili ya vitu usivyoweza kuvielezea. Unaamini kwamba siku moja dawa ya UKIMWI au saratani itapatikana mahali fulani, ilhali huwezi kufanya majaribio ya kisayansi kulithibitisha hilo. Unaweza kusubiri hata miaka mia, lakini kama bado dawa haijapatikana, unaweza kusubiri hata miaka mingine mia. Kuamini ni kujifanya kujua (na mara nyingi kujifanya kujua ni uongo) na kuamini hakuhitaji maarifa. Kujua kunahitaji maarifa na ni kuamini unakoweza kukuthibitisha. Ukiniuliza kama simu yangu ipo mfukoni nitakwambia ndiyo ipo, kwa sababu nitaingiza mkono mfukoni na kuitoa na kuiona. Siamini kama ipo mfukoni, najua. "
4 " Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani. "