Home > Topic > kujua
1 " Imani ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana na hupeleka watu kwenye ukweli. Kuamini hupotosha, na ni nia ya kudharau kinachoweza kujulikana. "
― Enock Maregesi
2 " Ukitaka kujua maana halisi ya maisha yako kuwa tayari kufanya vitu vikubwa vitakavyohitaji nguvu ya Mungu kuvikamilisha – na kudumu katika maisha hayo kwa kafara ya maombi. "
3 " Kuamini (mbali na imani, ambayo ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana) ni kwa ajili ya vitu usivyoweza kuvielezea. Unaamini kwamba siku moja dawa ya UKIMWI au saratani itapatikana mahali fulani, ilhali huwezi kufanya majaribio ya kisayansi kulithibitisha hilo. Unaweza kusubiri hata miaka mia, lakini kama bado dawa haijapatikana, unaweza kusubiri hata miaka mingine mia. Kuamini ni kujifanya kujua (na mara nyingi kujifanya kujua ni uongo) na kuamini hakuhitaji maarifa. Kujua kunahitaji maarifa na ni kuamini unakoweza kukuthibitisha. Ukiniuliza kama simu yangu ipo mfukoni nitakwambia ndiyo ipo, kwa sababu nitaingiza mkono mfukoni na kuitoa na kuiona. Siamini kama ipo mfukoni, najua. "