Home > Topic > kufanya
1 " Ukitaka kujua maana halisi ya maisha yako kuwa tayari kufanya vitu vikubwa vitakavyohitaji nguvu ya Mungu kuvikamilisha – na kudumu katika maisha hayo kwa kafara ya maombi. "
― Enock Maregesi
2 " Kuamini (mbali na imani, ambayo ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana) ni kwa ajili ya vitu usivyoweza kuvielezea. Unaamini kwamba siku moja dawa ya UKIMWI au saratani itapatikana mahali fulani, ilhali huwezi kufanya majaribio ya kisayansi kulithibitisha hilo. Unaweza kusubiri hata miaka mia, lakini kama bado dawa haijapatikana, unaweza kusubiri hata miaka mingine mia. Kuamini ni kujifanya kujua (na mara nyingi kujifanya kujua ni uongo) na kuamini hakuhitaji maarifa. Kujua kunahitaji maarifa na ni kuamini unakoweza kukuthibitisha. Ukiniuliza kama simu yangu ipo mfukoni nitakwambia ndiyo ipo, kwa sababu nitaingiza mkono mfukoni na kuitoa na kuiona. Siamini kama ipo mfukoni, najua. "
3 " Amri ya Kristo ilipima imani ya yule kipofu, ikiithibitisha na kuiimarisha. Bila kuchelewa au kusita, kipofu alitii amri ya Mungu: Alikwenda kuosha macho yake katika bwawa la Siloamu na aliona. Wengi wanaweza kuona ni kazi ya kipuuzi kwa mtu ambaye ni kipofu kufanya kazi ndogo kama hiyo ili aone. Lakini kwa vile alitii, kipofu alipona. Baraka huja kupitia utii. Kwa maana nyingine, kipofu alimtii Yesu bila kuona. Lakini matokeo yake, alipata kuona papohapo; ambapo baadaye, hatimaye, alipokea uponyaji halisi wa kiroho. "
4 " Kuna nguzo saba ambazo hazina budi kuzingatiwa kama unataka kuheshimiwa na kuwaheshimu wengine. Kwanza kabisa jitambue: wewe ni nani na unafanya nini hapa duniani. Halafu, kabla ya kusema jambo lolote kwa mtu yoyote fikiria kwanza maana au madhara ya hilo unalotaka kulisema. Kisha jifunze tamaduni mbalimbali na watendee wengine kama vile unavyotaka kutendewa au kama vile wanavyotaka kutendewa. Jifunze kusamehe na kusuluhisha migogoro katika jamii unamoishi huku ukidumisha heshima na utu kwa binadamu wenzako. Jijengee imani kwa watu, punguza upendeleo, fanya kazi kama timu kwani hakuna ‘mimi’ katika umoja ila kuna ‘sisi’, na jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE kwa manufaa ya wote. Kuwa kiongozi katika kila jambo unalofanya na katika kila kitu unachofanya. Jitahidi kufanya jambo au kitu kwa usahihi kwa kadiri utakavyoweza. "