Home > Author > Enock Maregesi >

" Wananchi wanapokosa huduma za muhimu za kijamii (kama vile afya, elimu, chakula, malazi, na ulinzi) ilhali wanalipa kodi, na wameajiri serikali kuwaendeshea nchi kwa kiapo cha uaminifu wa vitabu vitakatifu, watakosa imani na serikali yao! Vilevile wataathirika kiuchumi, kijamii na kisiasa, na vita itaweza kutokea kati ya wananchi na serikali, au wananchi kwa wananchi wataweza hata kujidhuru wenyewe – nikimaanisha vita ya wenyewe kwa wenyewe. Serikali ikifuata maadili ya kazi, na kuacha udikteta na urasimu wa aina yoyote ile, au ikifanya kazi kulingana na misingi ya katiba ya nchi; wananchi watapata huduma za kijamii kama wanavyostahili, na ndoto ya haki na ustawi wa jamii itaweza kutimia. Hata hivyo, serikali inaweza kuwadhulumu wananchi wake kwa sababu ya usalama wao. "

Enock Maregesi


Image for Quotes

Enock Maregesi quote : Wananchi wanapokosa huduma za muhimu za kijamii (kama vile afya, elimu, chakula, malazi, na ulinzi) ilhali wanalipa kodi, na wameajiri serikali kuwaendeshea nchi kwa kiapo cha uaminifu wa vitabu vitakatifu, watakosa imani na serikali yao! Vilevile wataathirika kiuchumi, kijamii na kisiasa, na vita itaweza kutokea kati ya wananchi na serikali, au wananchi kwa wananchi wataweza hata kujidhuru wenyewe – nikimaanisha vita ya wenyewe kwa wenyewe. Serikali ikifuata maadili ya kazi, na kuacha udikteta na urasimu wa aina yoyote ile, au ikifanya kazi kulingana na misingi ya katiba ya nchi; wananchi watapata huduma za kijamii kama wanavyostahili, na ndoto ya haki na ustawi wa jamii itaweza kutimia. Hata hivyo, serikali inaweza kuwadhulumu wananchi wake kwa sababu ya usalama wao.