Home > Author > Enock Maregesi >

" Lazima kuna mtu, si kitu, mwenye akili ya kupindukia, aliyeanzisha kila kitu kinachoonekana ulimwenguni. Mwaka 1995 wanasayansi waligundua kitu kilichowashtua kuliko kitu kingine chochote kile katika historia ya uwepo wao. Waligundua kuwa ulimwengu unaongeza mwendo wa kupanuka katika pande zote nne za ulimwengu – kwa mwendokasi wa maili milioni mbili kwa saa! Nini kinasababisha ulimwengu uongeze mwendo kiasi hicho badala ya kuupunguza? Ni nini hicho ambacho ulimwengu unapanukia? Mpaka sayansi ijibu maswali hayo na mengineyo mengi, kama vile kitendawili cha ‘standard model’ na chembe ya ‘boson’ inayofanya kila kitu ulimwenguni kuwa na uzito, nitaendelea kuamini kuna Mtu anayesababisha yote hayo kutokea. "

Enock Maregesi


Image for Quotes

Enock Maregesi quote : Lazima kuna mtu, si kitu, mwenye akili ya kupindukia, aliyeanzisha kila kitu kinachoonekana ulimwenguni. Mwaka 1995 wanasayansi waligundua kitu kilichowashtua kuliko kitu kingine chochote kile katika historia ya uwepo wao. Waligundua kuwa ulimwengu unaongeza mwendo wa kupanuka katika pande zote nne za ulimwengu – kwa mwendokasi wa maili milioni mbili kwa saa! Nini kinasababisha ulimwengu uongeze mwendo kiasi hicho badala ya kuupunguza? Ni nini hicho ambacho ulimwengu unapanukia? Mpaka sayansi ijibu maswali hayo na mengineyo mengi, kama vile kitendawili cha ‘standard model’ na chembe ya ‘boson’ inayofanya kila kitu ulimwenguni kuwa na uzito, nitaendelea kuamini kuna Mtu anayesababisha yote hayo kutokea.