Home > Author > Enock Maregesi >

" Kuna mambo yanatokea hapa ulimwenguni ambayo yanafanya nikiri uwepo wa Mungu kwa asilimia kubwa. Wanasayansi wanasema ulimwengu ulianzishwa na mlipuko wa ‘Big Bang’, uliotokea takribani miaka bilioni 14 iliyopita, kutoka katika kitu kidogo zaidi kuliko ncha ya sindano, lakini hawatuambii nini kilisababisha mlipuko huo utokee au hicho kitu kidogo kuliko ncha ya sindano kilitoka au kilikuwa wapi.

Wanaendelea kusema kuwa baada ya ‘Big Bang’ kutakuwepo na ‘Big Crunch’, ambapo ulimwengu utarudia hali yake ya awali ya udogo kuliko ncha ya sindano, na kila kitu kinachoonekana leo ulimwenguni hakitaonekana tena.

Hapo sasa ndipo utata unapokuja. Mlipuko wa ‘Big Bang’ ulipotokea ulimwengu ulilipuka na kusambaa pande zote nne za ulimwengu kwa mwendokasi wa zaidi ya kilometa milioni 2 kwa saa, mpaka hivi leo unavyoonekana na bado unaendelea kusambaa. Kutokana na dhana ya ‘Big Crunch’, wanasayansi wanaamini ulimwengu utapanuka ila baadaye utapungua mwendo na utarudi mwanzo kabisa mahali ulipolipukia.

Lakini mwaka 1995 wanasayansi hao hao waligundua kitu. Ulimwengu – badala ya kupungua mwendo wa kupanuka kama wanasayansi walivyokuwa wakitabiri – sasa unaongeza mwendo, tena kwa mwendokasi ambao haujawahi kutokea.

Hiki ni nini kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kiasi hicho badala ya kuupunguza? Hicho ni nini ambacho ulimwengu unapanukia? Wanasayansi hawana jibu. Wanasingizia kitu kinaitwa ‘dark matter’, maada ambayo haijawahi kuonekana, kwamba ndicho kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kwa kiwango hicho ambacho hakijawahi kutokea; na hicho ambacho ulimwengu unapanukia wanahisi ulimwengu wetu unapanukia katika ulimwengu mwingine, kwa mujibu wa dhana nyingine kabisa iitwayo ‘multiverse’ au ‘meta-universe’.

Kuna kitu kinaitwa ‘Higgs boson’ – chembe ndogo inayosemekana kuhusika na uzito (‘mass’) wa chembe ndogo 16 zilizomo ndani ya atomu, kasoro chembe ya mwanga, iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa ‘Big Bang’ miaka bilioni 13.7 iliyopita katika kipindi kilichoitwa ‘epoch’ – ambayo ilianza kutafutwa katika maabara za CERN, Uswisi, toka mwaka 1964, maabara ambazo kazi yake kubwa ni kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa ‘Big Bang’, kusudi wanasayansi waone kama wanaweza kubahatisha kuiona na kuidhibiti hiyo bosoni.

Bosoni itakapopatikana wanasayansi watajua siri ya ‘dark matter’, watajua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa na jibu la kitendawili cha ‘Standard Model’ litapatikana.

Hiyo ni kazi ngumu. Ndiyo maana ‘Higgs boson’ mwaka 1993 iliitwa ‘The God Particle’. Yaani, wanasayansi wanahisi kuna muujiza wa Kimungu na huenda wasiipate kabisa hiyo bosoni. Wanasema waliipata mwaka 2013. Lakini hiyo waliyoipata bado ina utata.

Kutokana na kushindwa huko kwa sayansi na historia, kutokana na kushindwa kwa sayansi kutengeneza binadamu au mnyama, kutokana na miujiza iliyorekodiwa katika vitabu vitakatifu; naamini, Mungu yupo. "

Enock Maregesi

Image for Quotes

Enock Maregesi quote : Kuna mambo yanatokea hapa ulimwenguni ambayo yanafanya nikiri uwepo wa Mungu kwa asilimia kubwa. Wanasayansi wanasema ulimwengu ulianzishwa na mlipuko wa ‘Big Bang’, uliotokea takribani miaka bilioni 14 iliyopita, kutoka katika kitu kidogo zaidi kuliko ncha ya sindano, lakini hawatuambii nini kilisababisha mlipuko huo utokee au hicho kitu kidogo kuliko ncha ya sindano kilitoka au kilikuwa wapi.

Wanaendelea kusema kuwa baada ya ‘Big Bang’ kutakuwepo na ‘Big Crunch’, ambapo ulimwengu utarudia hali yake ya awali ya udogo kuliko ncha ya sindano, na kila kitu kinachoonekana leo ulimwenguni hakitaonekana tena.

Hapo sasa ndipo utata unapokuja. Mlipuko wa ‘Big Bang’ ulipotokea ulimwengu ulilipuka na kusambaa pande zote nne za ulimwengu kwa mwendokasi wa zaidi ya kilometa milioni 2 kwa saa, mpaka hivi leo unavyoonekana na bado unaendelea kusambaa. Kutokana na dhana ya ‘Big Crunch’, wanasayansi wanaamini ulimwengu utapanuka ila baadaye utapungua mwendo na utarudi mwanzo kabisa mahali ulipolipukia.

Lakini mwaka 1995 wanasayansi hao hao waligundua kitu. Ulimwengu – badala ya kupungua mwendo wa kupanuka kama wanasayansi walivyokuwa wakitabiri – sasa unaongeza mwendo, tena kwa mwendokasi ambao haujawahi kutokea.

Hiki ni nini kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kiasi hicho badala ya kuupunguza? Hicho ni nini ambacho ulimwengu unapanukia? Wanasayansi hawana jibu. Wanasingizia kitu kinaitwa ‘dark matter’, maada ambayo haijawahi kuonekana, kwamba ndicho kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kwa kiwango hicho ambacho hakijawahi kutokea; na hicho ambacho ulimwengu unapanukia wanahisi ulimwengu wetu unapanukia katika ulimwengu mwingine, kwa mujibu wa dhana nyingine kabisa iitwayo ‘multiverse’ au ‘meta-universe’.

Kuna kitu kinaitwa ‘Higgs boson’ – chembe ndogo inayosemekana kuhusika na uzito (‘mass’) wa chembe ndogo 16 zilizomo ndani ya atomu, kasoro chembe ya mwanga, iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa ‘Big Bang’ miaka bilioni 13.7 iliyopita katika kipindi kilichoitwa ‘epoch’ – ambayo ilianza kutafutwa katika maabara za CERN, Uswisi, toka mwaka 1964, maabara ambazo kazi yake kubwa ni kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa ‘Big Bang’, kusudi wanasayansi waone kama wanaweza kubahatisha kuiona na kuidhibiti hiyo bosoni.

Bosoni itakapopatikana wanasayansi watajua siri ya ‘dark matter’, watajua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa na jibu la kitendawili cha ‘Standard Model’ litapatikana.

Hiyo ni kazi ngumu. Ndiyo maana ‘Higgs boson’ mwaka 1993 iliitwa ‘The God Particle’. Yaani, wanasayansi wanahisi kuna muujiza wa Kimungu na huenda wasiipate kabisa hiyo bosoni. Wanasema waliipata mwaka 2013. Lakini hiyo waliyoipata bado ina utata.

Kutokana na kushindwa huko kwa sayansi na historia, kutokana na kushindwa kwa sayansi kutengeneza binadamu au mnyama, kutokana na miujiza iliyorekodiwa katika vitabu vitakatifu; naamini, Mungu yupo.