Home > Author > Enock Maregesi >

" Potassium Cyanide si hatari inapokuwa nje. Ni hatari inapojichanganya na asidi za tumboni ambapo hubadilika na kuwa gesi ya 'hydrogen cyanide'. Gesi ya 'hydrogen cyanide' ni miongoni mwa sumu hatari zaidi ulimwenguni. Mtu akimeza kidonge cha 'cyanide' atapata madhara makubwa. Kichwa chake kitamuuma hapohapo na atachanganyikiwa akili. Ngozi yake itakuwa nyekundu, kwa sababu damu yake itakuwa nyekundu zaidi – kutokana na kuzidi kwa oksijeni katika damu. Mwili hautakuwa na uwezo tena wa kuchukua oksijeni kutoka katika damu ili uitumie, kwa hiyo damu itazidi kuwa na oksijeni zaidi. Atapumua kwa shida. Mapafu yake yatafanya kazi vizuri lakini mwili wake hautakuwa na uwezo wa kutumia oksijeni yoyote – hivyo atadhani ana matatizo katika mfumo wake wa kupumua. Atazimia. Yaani, oksijeni haitafika kwenye ubongo. Atapata kifafa na atatapika nyongo. Ubongo wake utashindwa kufanya kazi na atakuwa mahututi ndani ya sekunde kumi! Baada ya hapo moyo wake utasimama kufanya kazi, na atafariki dunia. "

Enock Maregesi


Image for Quotes

Enock Maregesi quote : Potassium Cyanide si hatari inapokuwa nje. Ni hatari inapojichanganya na asidi za tumboni ambapo hubadilika na kuwa gesi ya 'hydrogen cyanide'. Gesi ya 'hydrogen cyanide' ni miongoni mwa sumu hatari zaidi ulimwenguni. Mtu akimeza kidonge cha 'cyanide' atapata madhara makubwa. Kichwa chake kitamuuma hapohapo na atachanganyikiwa akili. Ngozi yake itakuwa nyekundu, kwa sababu damu yake itakuwa nyekundu zaidi – kutokana na kuzidi kwa oksijeni katika damu. Mwili hautakuwa na uwezo tena wa kuchukua oksijeni kutoka katika damu ili uitumie, kwa hiyo damu itazidi kuwa na oksijeni zaidi. Atapumua kwa shida. Mapafu yake yatafanya kazi vizuri lakini mwili wake hautakuwa na uwezo wa kutumia oksijeni yoyote – hivyo atadhani ana matatizo katika mfumo wake wa kupumua. Atazimia. Yaani, oksijeni haitafika kwenye ubongo. Atapata kifafa na atatapika nyongo. Ubongo wake utashindwa kufanya kazi na atakuwa mahututi ndani ya sekunde kumi! Baada ya hapo moyo wake utasimama kufanya kazi, na atafariki dunia.